Of love & other drugs pt3

Sio ati amenikataa lakini pia hajasema ndio

Ju  ametoka bara sitaki kumpeleka mbio

Moyoni nadai kumwambia ‘jaber tim piyo’

Yani mrembo harakisha unizimie kisha 

Uwe my Cole like Keysha hata Kama budako anatisha

Hakuna mwingine nataka katika hii maisha

Nataka mi na we tuwe pamoja’ . 

Najua hapo atasema ‘kaka, ngoja

Sitaki mwanaume amejaa pomoni na vioja

Na Kama wako mimi sio nambari moja

Kuwa Jonny walker, endelea kutembea’

Niko na mafua ya mapenzi na ye ndio tembe ya

Kunitibu.sisemi mi ni yesu lakini nimemkufia 

Six months down the line bado box hajaingia

Nilimuuliza Kama anatuona pamoja katika siku za usoni

Akasema ye haeziona mbali bila miwani usoni

Hata Kama subira huvuta heri naona ni heri

Nimwambie maze kwaheri na nakutakia kilalaheri 

Penzi lako ni bahari nafaa kuvuka na sina feri

Nitazama. Nikimtazama naskia sauti ya mama

Ikisema nisichoke kukazana hata kama amenikaza na 

Kamba shingoni niendelee kusimama Kama mlinzi mlangoni

Siku za mwizi ni arubaini na vile ameiba moyo wangu nina tumaini

Siku zake zinakaribia kuisha nitamshika na sitaachilia bila kubaini

Kuwa hanipendi kwa kipimo kilekile au yeye ni gaidi

Wa mapenzi na kila uchao ninavyozidi kumuenzi

Napiga dua neno pendo ataligeuza kuwa kitenzi
Copyright Paul Zay 2017

Advertisements

2 thoughts on “Of love & other drugs pt3

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s